TAJIRI "ANAEMPA ZUMA KIBURI" AVAMIWA - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Wednesday, February 14, 2018

TAJIRI "ANAEMPA ZUMA KIBURI" AVAMIWA

Members of the Hawks special police unit stand guard outside Gupta home
Kikosi cha "The Hawks" kikifanya doria kwenye makazi ya Gupta (Picha AFP)

Watu watatu wamekamatwa baada ya nyumba ya familia ya Gupta yenye utata nchini Afrika Kusini kuvamiwa katika muendelezo wa uchunguzi dhidi ya familia hiyo inayodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali.
Familia tajiri ya wazaliwa wa India ya Gupta imeshutumiwa kwa kutumia urafiki wao na Rais Zuma kwa manufaa binafsi na kibiashara.
Bwana Zuma na wakina Gupta wote wamekana shutuma hizo dhidi yao.
Tens of thousands of South Africans from various political and civil society groups march to the Union Buildings to protest against South African president and demand his resignation on April 7, 2017 in Pretoria.
Maandamaon ya Kumpinga Guta  na Zuma(Picha ya AFP)
Kwa kiasi shinikizo kubwa la Zuma kujiuzulu linatokana na uhusiano wake na familia hiyo.
Anatarajiwa kuzungumza hivi karibuni kuhusu wito wa chama cha ANC wa kuondoka madarakani.
Cheo cha Zuma kama kiongozi wa chama kilichukuliwa na makamu wake, Cyril Ramaphosa, Disemba mwaka jana ,lakini hadi sasa amekataa wito wa chama kujiuzulu.
Afisa mmoja wa chama amesema alikuwa tayari kuachia ngazi ndani ya miezi mitatu hadi sita ijayo, lakini viongozi wa juu wanataka atoke mara moja.
Kiongozi huyo mwenye kashfa nyingi amekuwa madarakani tangu mwaka 2009.
Kikosi maalum cha 'The Hawks', kimethibitisha wamezingira eneo la Gupta mjini Johannesburg Jumatano asubuhi
Familia ya Gupta inayomiliki baadhi ya biashara Afrika Kusini imeshutumiwa kutumia ushawishi wao na urafiki na Jacob Zuma vibaya kupata mikataba ya serikali inayogharimu mamilioni ya dola za kimarekani.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo