![]() |
Kamanda wa Polisi Kanad Maalum ya Dar es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa |
Jeshi la Polisi: Habari iliyoandikwa na Gazeti la Nipashe kwamba “Polisi wanawakamata wavaa vimini na wanyoa viduku” imepikwa, si ya kweli!
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa habari zllizochapishwa na gazeti hilo hazina ukwel wowote
ACP Mambosasa amesema kuwa mwandishi (na gazeti lake) wanatafuta umaarufu kwa kutengeneza habari za kupika.
Aidha Mambosasa ameongeza kuwa mwandishi amesema kuwa hakuna msako wowote wa aina hiyo bali wanachofanya ni kukama ta watu wanaovunja na kukiuka maadili ya Kitanzania.
"Mtu anaweza kufanya jambo la kuudhi ila hakuvuja sheria" amesema Mambosasa.
Kamanda huyo amemtaka mwandishi huyo awaombe radhi Watanzania
Hivi karibuni gazeti hilo "Nipashe Jumapili "liliomba radhi na na kujfungia lenyewe kwa kuchapisha habari za Uongo dhidi ya Rais Dk. John Magufuli
No comments:
Post a Comment