Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Dkt Augusrine Mahiga |
Mabalozi hao wameahidi
mataifa yao yatachangia kuisaidia Tanzania kwa vifaa vya kisasa na mafunzo ya
kuweza kufuatilia mienendo ya meli inazozipatia usajili.
Juma
moja lililopita Rais wa Marekani Donald Trump alitishia kuyawekea vikwazo vya
Kiuchumi Kidplomasia Kisiasa na kibiashara mataifa yote yatakayokiuka vikwazo
vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa na Marekani kwa Korea ya Kaskazini ikiwa ni
kuweka mkwamo kwa mpango wake wa kustawisha silaha za nyuklia.
Meli hizo zilizokuwa
zikipeperusha bendera ya Tanzania zilionekana kwa njia ya setilaiti, moja
ikielekea Korea ya Kaskani moja kwa moja na nyingine ilinaswa ikihamisha mizigo
ambayo haikutambulika kwenye meli nyingine ambayo baada ya zoezi hilo la
uhamishaji ilielekea Korea ya Kaskazini baada ya kupakia mizigo hiyo.
Mwezi
wa kwanza mwaka huu Tanzania ilizifutia usajili meli zote 450 zilizokuwa
zinapeperusha bendera yake kwenye maji ya kimataifa ikiwa ni baada ya
kupatikana kwa meli iliyokuwa imebeba shehena ya silaha na dawa za kulevya huku
ikipeperusha bendera ya Tanzania.
Tangu
kufutwa kwa usajili huo uchunguzi uliofanyika tayari umebaini meli 119
zimetenda makosa mbali mbali ikiwemo kupeleka bidhaa kwenye nchi zenye vikwazo,
kubeba silaha na dawa za kulevya, na kubeba mafuta ya wizi
No comments:
Post a Comment