Polisi wakiweka kizuizi kwenye eneo la Ikulu ya White House |
Kikosi
hicho kilisema kuwa mwanamume huyo
ambaye jina lake bado halijatangazwa alikaribia uzio unaozunguka Ikulu katika barabara ya
Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.
Rais Donald Trump hakuwa
kwenye Ikulu. Na alikuepo katika kasri
lake la Mar-a-Lago huko Florida.
Mwanamume huyo alikuwa
kwenye watu wengi wakati alipiga risasi, kulingana na na mashuhuda wa tukio
hilo.
Video iliyochapishwa
kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo.
Kumekuwa na visa kadha
vinavyohusu usalama katika Ikulu ya White House miaka ya hivi karibuni.
Tukio
la hivi hivi karibuni tarehe 23
Februari, gari liliendeshwa kwenda kwa kizuizi cha Ikulu ambapo mwanamke wa
miaka 35 alikamatwa.
No comments:
Post a Comment