Mtu
mmoja mkazi wa Nyegezi jijini Mwanza, Bw. Soli Mkanzabe (24), anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumbaka na
kumjeruhi sehemu za siri mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa).
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo la
jinai Februari 26, mwaka huu, saa 10 jioni katika mtaa wa Password.
"Inadaiwa
mtuhumiwa alifika nyumbani kwao mtoto huyo na kumkuta akicheza na wenzake
akamwita waende chumbani kwake," amesema Kamanda Msangi na kuendelea:
"Mtoto
alimfuata kwenda chumbani na baadaye mtuhumiwa alimfanyia ukatili wa kumbaka na
kumsababishia maumivu makali sehemu za siri, huku akimuonya asiseme kwa mtu
yeyote jambo hilo."
Amesema,
baada ya mtoto huyo kufanyiwa ukatili huo, hakumwambia mtu, lakini mama yake
aliporudi kutoka kazini alimuogesha na kugundua amebakwa, ndipo alitoa taarifa
kituo cha Polisi.
"Polisi
walifanya ufuatiliaji haraka eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Wanaendelea kupeleleza na kumhoji mtuhumiwa. Uchunguzi ukikamilika atafikishwa
mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake," amesema Msangi.
Mtoto huyo
alipatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na hali yake inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment