AKILI ZA TRUMP HAZINA MATATIZO- DATARI - NIJUZE NEWS

Breaking news

Nyumba ya Habari Makini na za Uhakika

Pata Habari Mpya kwa kina Kila muda kutoka kwanye vyanzo vya Uhakika

Mikoani leo

Mikoani leo

Wednesday, January 17, 2018

AKILI ZA TRUMP HAZINA MATATIZO- DATARI

Image result for picha za Trump
Donald Trump, Rais wa Marekani
Ikulu ya Marekani ya  White House imesemaa kuwa Rais wa nchi hiyo Donald  Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi wa kiafya na yuko na afya nzuri,.
"Sina wasi wasi wowote kuhusu afya ya akili ya Trump," Ronny Jackson alisema Jumanne.
Wiki iliyopita  Rais Trump alifanyiwa uchunguzi wa afya wa saa tatu, ambao ni wake wa kwanza tangu awe rais wa Marekani.
White House physician Ronny Jackson answers question about US President Donald Trump's health after the president's annual physical at the White House in Washington, 16 January 2018
Dkt Ronny Jackson(Picha ya Reuters)
Hii ni baada ya kutolewa kitabu chenye utata kulichoeneza uvumi kuhusu afya ya kiakili ya Rais Trump.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano huko White House, Dkt Jackson alisema kuwa kwa jumla afya ya rais ni nzuiri.
"Anaendelea kufurahia moyo wenye afya na afya yote kwa jumla kutokana na kutovuta sigara na kutokunywa pombe," ameongzea Dkt. huyo
Hata hivyo Dkt Jakcson amesema kuwa Bw. Trump, 71, atanufaika kwa kupunguza vyakula vyenye mafuta na mazoezi zaidi.
Siku ya Ijumaa rais alichunguzwa na madaktari wa kijeshi katika kituoa cha afya cha Walter Reed huko Bethesda, Maryland katika uchunguzi uliotajwa kuwa uliofanikiwa.
Kulingana na Michael Wolf ambaye ni mwandishi wa kitabu cha Fire and Fury: Inside the Trump White House, ni kuwa wafanyakazi wote wa White House walimuona Trump kama mtoto.
Trump alijibu kwa kusema kwa kitabu hicho kimejaa uongo huku naye waziri wa mashauri ya nchi za kigeni akikana madai kuwa afya ya rais ilikuwa inafeli.

No comments:

Post a Comment

Mikoani leo

Mikoani leo